Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ali Shamkhani amesema hayo katika ujumbe alioutuma mapema leo kwenye ukurasa wa Twitter na kubainisha kuwa, "kuendeleza marufuku ya silaha dhidi ya Iran muda wake ukitamatika kutakuwa ni ukiukaji wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la UN."
Amezihutubu nchi za Ulaya kwa kusema, "Ulaya inasimama upande gani? Je itadumisha hadhi na heshima na kuimarisha maamuzi ya pande kadhaa, au itakubali kudhalilishwa na kuunga mkono uamuzi wa upande mmoja?"
Ali Shamkhani amesisitiza kuwa, lengo la Marekani la kushupalia mkakati wake wa mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Iran ni kuyumbisha irada na imani ya mrengo imara na unaopambana na uistikbari wa dunia.
Amesema 'virusi vya vikwazo' ni chombo kinachotumiwa na Ikulu ya White House ya Marekani kujaribu kuubakisha hai utawala wa kiistikbari wa Marekani unaoporomoka.
Baada ya Baraza la Usalama la UN kupitisha mapatano ya JCPOA, iliafikiwa kuwa Oktoba 18 mwaka 2020 Iran itaondolewa vikwazo vya silaha kwa ridhaa ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, jambo ambalo linaikera Washington.
342/